Robertinho: Makundi CAF kitawaka!

DSM: HIVI sasa mtaani pamoja na makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii mjadala ni kuhusu droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopangwa leo nchini Afrika Kusini kuhusu makundi waliyopangwa Simba na Yanga za Tanzania.

Kila mmoja anasema lake, wapo wanaojifariji kwa namna mbalimbali lakini mioyo inadunda, lakini wapo ambao kiukweli wamefurahia na wapo ambao hawajiamini kabisa.

Simba yenyewe imepangwa Kundi B na timu za Wydad Casablanca ya Morocco, Asec Mimosas ya Ivory Coast na Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Sasa ipo hivi, wakati mashabiki wakiendelea na mijadala yao, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, naye alitulia akawa anafuatilia upangaji huo wa makundi na kusema licha ya ugumu wa michezo hiyo hatua ya makundi lakini wanajua jinsi ya kutimiza malengo yao.

“Kila mmoja wetu anatambua jinsi gani ambavyo tuna michezo mikubwa na migumu mbeleni, ila kwangu kama kocha, wachezaji na viongozi tunajua njia bora ya kutimiza malengo yetu ni maandalizi,” amesema Robertinho.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Charles Lyimo
Charles Lyimo
1 month ago

ngoja tusubiri

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x