Robertinho: Tunataka heshima

Inaweza kuwa ni taarifa Chungu kwa maafande wa Ruvu shooting baada ya kocha mkuu wa Simba Roberto Oliviera ‘ Roberthno’ kusema kwamba wanataka kushinda mchezo utakopigwa kesho Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Ruvu shooting.

Robertnho amesema haijalishi kuwa watavuna nini mwisho wa msimu lakini wanachotaka ni kuilinda heshima ya timu.

“Sio mchezo mrahisi kwetu lakini ni lazima tushinde, nimewaambia wachezaji wangu kuwa tunapaswa kumaliza vizuri msimu na mashabiki zetu.”amesema┬áRobertnho

Kocha msaidizi wa Ruvu shooting, Frenk Msise amesema bado hawajakata tamaa wanaamini inawezekana wao kusalia kwenye ligi kwa msimu ujao.

“Kwa uzoefu tulionao tunaamini kwenye michezo mitatu iliyosalia tunaweza kupata matokeo na kusalia kwenye ligi kwa msimu ujao, simba wametuzidi katika uwekezaji ila hakuna aliyejua kama Simba atamfunga Wydad kwahiyo hata sisi tunaamini tunaweza kushinda” amesema Mzize

Mpaka sasa Ruvu shooting inaburuza mkia katika ligi hiyo ikiwa na alama 20 hivyo hesabu zao ni kushinda dhidi ya Simba ili kujinusuru na jinamizi la kushuka daraja.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button