Roberto Martinez kocha mpya Ureno

Kocha wa zamani wa Ubelgiji Roberto Martinez ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Ureno, shirikisho la soka nchini humo (FPF) limethibitisha.

“Ninashukuru shauku na tamaa ambayo yeye (Martinez) alipokea mwaliko,” rais wa FPF Fernando Gomes aliambia mkutano wa waandishi wa habari. “Huu ni wakati muhimu kwa timu ya taifa.”

Martinez ameteuliwa kuifundisha timu hiyo ikiwa ni mwezi mmoja tangu kuachana na Ubelgiji mara baada ya kuondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Kocha huyo anachukuwa nafasi ya Fernando Santos ambaye aliikacha Ureno mara baada ya Kombe la Dunia kutokana na kufanya vibaya

Habari Zifananazo

Back to top button