KIUNGO mkabaji wa Manchester City, Rodrigo Cascante ‘Rodri’ ameumia na kulazimika kuondoka uwanjani katika mchezo dhidi ya Fluminence mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia.
Rodri ameonekana akiugulia maumivu ya goti, na hivyo kulazimika kuondolewa uwanjani.
Hata hivyo inasubiriwa ripoti ya madaktari wa City kuona ni kwa kiasi gani majeraha hayo yana ukubwa.
Licha ya kuumia kwa Rodri pia taarifa njema ni urejeo wa kiungo mshambuliaji Kevin De Bruyne.