Roma waachana na Mourihno

KLABU ya AS Roma imethibitisha kuachana na kocha Jose Mourinho kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo imeeleza kuwa Mourinho anaondoka jijini Roma na benchi lake la ufundi.

Mreno huyo alitua kwa Giallorossi akiwa kocha wa 60 wa klabu hiyo mwezi Mei 2021.

Mourinho aliisaidia Roma kushinda ubingwa wa Conference League huko Tirana Mei 2022 na Kombe la Europa huko Bundapest.

“Tungependa kumshukuru Jose kwa niaba yetu sote hapa Roma kwa juhudi zake tangu alipowasili klabuni hapa.” Imeeleza taarifa ya Roma.

Habari Zifananazo

Back to top button