IMEELEZWA kuwa mshambuliaji wa Al Nassr FC, Cristiano Ronaldo anataka kuondoka klabuni hapo licha ya sababu kutotajwa huku akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili. Mtandao wa Sky Sport umeeleza.
Ronaldo alijiunga na klabu hiyo ya Saudi Arabia akitokea Manchester United.
Nahodha huyo wa Ureno alikubali kusitisha mkataba wake na United baada ya mahojiano yake na Mwandishi wa Habari Piers Morgan, licha ya uwepo wa taarifa za kutokuwa na maelewo mazuri na uongozi wa timu hiyo na kocha Eric Ten Hag.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 kisha alikubali mkataba wa pauni milioni 175 kwa mwaka hadi 2025 na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.
Comments are closed.