Ronaldo ala nyekundu kwa kupiga

Abu Dhabi, UAE: NAHODHA wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo alitolewa nje kwa kadi nyekundu, baada ya timu yake kufungwa 2-1 na wapinzani wao Al Hilal katika nusu fainali ya Saudi Super Cup jana mjini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE).

Mfungaji huyo bora wa Ureno alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika nne kabla ya mechi kumalizika kwa kumpiga kiwiko mpinzani wakati timu yake ilipolala 2-1.

Al Hilal wanatafuta taji la nne katika mechi ya fainali watakayokipiga Alhamisi dhidi ya Al Ittihad ya Karim Benzema, ambao waliilaza Al Wehda 2-1 katika nusu fainali ya mapema iliyopigwa Jumatatu iliyopita.

Advertisement

Ronaldo alijiunga na Al Nassr, Desemba 31, 2022, mkataba wake ni miaka miwili na nusu. Alianza kuichezea Al Nassr Januari 2023, bado hajashinda kombe la soka nchini Saudi Arabia.