Ronaldo aondoka Man U

Manchester United imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Cristiano Ronaldo.
Iliripotiwa wiki iliyopita kuwa United walikuwa wameanza mchakato wa kisheria dhidi ya Ronaldo kwa kuvunja mkataba baada ya mahojiano yake na Piers Morgan.
Kazi hiyo imeendelea kwa kasi na sasa Ronaldo mwenye miaka 37 ameondoka United.