Ronaldo augua, akosa mazoezi

TAARIFA kutoka katika kambi ya Ureno zinaelezakuwa mshambuliaji wa timu hiyo na Manchester United, Cristiano Ronaldo ameshindwa kufanya mazoezi na kikosi hicho kinachojiandaa na mashindano ya Kombe la Dunia kutokana na kusumbuliwa na tumbo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alikosa mechi mbili zilizopita za Manchester United dhidi ya Aston Villa na Fulham kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa.

Ronaldo amegonga vichwa vya habari siku za hivi karibuni baada ya kushiriki katika mahojiano na Piers Morgan, na taarifa zaidi za mahojiano hayo ya kwanza yataonyeshwa kwenye TalkTV leo na kesho usiku.

Katika mahojiano ambayo Morgan ameyaweka hadharani amesikika Ronaldo akiwaongela vibaya baadhi ya viongozi wa United, akiwemo kocha Eric Ten Hag ambaye alisema hawezi kumheshimu kwa kuwa yeye hamheshimu.

Ronaldo alienda mbali zaidi na kusema kuwa tangu kuondoka kwa kocha wa zamani wa timu hiyo, Alex Ferguson timu hiyo haijapiga hatua na haina maendeleo mpaka sasa. Alisema kuwa baadhi ya miundombinu haijafanyiwa maboresho tangu alipoondioka kwenda Real Madrid mwaka 2008.

Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa timu ya Manchester United ambao wanaichezea Ureno akiwemo Bruno Fernandez na Diogo Dalot wameoneka kwenye baadhi ya video wakiwa hawana furaha na mchezaji huyo na kuzua sintofahamu hata wanaposalimiana.

Habari Zifananazo

Back to top button