Ronaldo ndio basi tena Ulaya

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amefuta uwezekano wa kurejea tena kusakata soka barani Ulaya na kusema ligi ya Saudi Arabia ni bora kuliko ligi ya Marekani ambayo nyota Lionel Messi amejiunga nayo.

Kwa mujibu mtandao wa ESPN kauli hiyo imekuja mara baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Celtavigo ambapo timu yake ilibugizwa bao 5-0.

“Nina uhakika wa 100% siwezi kurudi kwenye klabu yoyote barani Ulaya nina miaka 38 kwa sasa, Mpira wa Ulaya umepoteza ladha yake ligi ambayo inafanya vizuri na ina ubora kwa sasa ni ligi kuu ya England pekee” alinukuliwa Ronaldo

Ronaldo ameongeza kuwa Ligi ya Saudi Arabia ni bora kuliko ligi ya Marekani na ndio sababu wachezaji wengi wakubwa wanatimkia huko Saudi Arabia na anamini ndani ya mwaka mmoja ligi hiyo itapasua anga zaidi na kuzipita baadhi ya ligi za Ulaya.

Mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora ulimwenguni Ballon dior mara tano alijiuunga na Al Nassr in Desemba 2022 baada ya kuachana na Manchester United na baada ya uhamisho wake nyota wengi wanatua kwenye ligi hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button