Ronaldo ng’ombe asiyezeeka maini

JEDDAH, Saudi Arabia: AKIWA na umri wa miaka 38 ndani ya jezi ya Al Nassr, Cristiano Ronaldo anaongoza kwa upachikaji mabao kwa mwaka 2023.

Amefunga 53, pasi za mabao 15 ndani ya mechi 58 pekee.

Wanaomfuatia katika ufungaji ni Kylian Mbappe, mabao 52 katika michezo 53 ndani ya uzi wa Paris Saint-Germain akiwiana na mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane mwenye magoli 52 katika mechi 57.

Ilhali, Erling Haaland akiwa na jumla ya mabao 50 katika mechi 60 ndani ya Manchester City.

Al Nassr ya Ronaldo ipo nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League), ikiwa na alama 43, alama Saba nyuma ya vinara Al Hilal yenye alama 50, wakiwa tayari wameshuka dimbani mara 18.

 

Habari Zifananazo

Back to top button