Ronaldo waajabu akataa tuta.

CRISTIANO Ronaldo ameonesha uungwana kwa kukataa penalty aliyopewa na mwamuzi baada ya kujiangusha eneo la hatari katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Asia kati ya Al-Nassr na Persepolis ya Iran.

Ronaldo alianguka eneo la hatari kipindi cha kwanza na mwamuzi Ma Ning kuonesha ishara ya penalty, wakati wachezaji wa Persepolis wakimlalamikia mwamuzi, Ronaldo aliungana nao kukataa adhabu hiyo.

Baada ya Ronaldo kufanya hivyo na wachezaji pinzani, mwamuzi huyo aliangalia marudio ya tukio la kubatilisha maamuzi yake.

Katika mchezo huo ulioisha suluhu, Al-Nassr walimaliza pungufu baada ya beki Ali Lajimi kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza kwa kumchezea vibaya Milad Sarlak.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button