MSANII wa kike anayefanya vizuri kwenye muziki wa Hip Hop, Rosary Robert ‘Rosa Lee’ (pichani) amesema kuwa Christian Bella sio mtu wa kawaida kwenye maisha yake, kwani amekuwa nguzo muhimu kwake hadi hapo alipofika kutokana na ushauri anaompa.
Rosa Lee hivi sasa anatamba na albamu yake ya kwanza alioipa jina la Goddes aliyoiachia wiki iliyopita, ambayo inafanya vizuri kwenye chati mbalimbali za muziki za ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa kutokana na ukongwe wake kwenye muziki umemfanya ajifunze vitu vingi kutoka kwake na amekuwa akimpa ushauri wa kumjenga ili aweze kufikia malengo yake.
“Unajua Bella ni msanii mkubwa amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu ni kaka ambaye namheshimu sana kutokana na kile amekuwa akikifanya kwangu,” alisema Rosa Lee.
kuwa kitendo cha kumsindikiza siku ya uzinduzi wa albamu yake inaonyesha wazi upendo wake kwake kitu kinachofanya ajione mwenye bahati kuwa karibu na mkongwe huyo wa muziki wa dansi.