Rose Muhando kuachia albamu mpya

MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa Injili nchini Rose Mhando kuachia album yake mpya kabla ya mwaka huu kuisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, tayari ameachia orodha ya nyimbo (tracklist) za album hiyo ijayo ambayo ameipa jina “Secret Agenda”. Tarehe rasmi ya kuitoa ataitoa hivi karibuni.

Album hiyo ina jumla ya nyimbo 12, huku wimbo namba 5 katika album hiyo ni “Secret Agenda” ambao ndio umebeba jina la album.

Advertisement

Kaa tayari kwa album hiyo mpya ya Malkia Rose Mhando ambayo itazifuata album zake nyingine kama ‘Mteule Uwe Macho’, ‘Kitimutimu’, ‘Jipange Sawasawa’ na ‘Utamu wa Yesu’.