Roy Kean: Bruno avuliwe unahodha

KUMEKUCHA huko Manchester, mkongwe wa zamani wa Manchester United, Roy Keane anataka kiungo wa timu hiyo, Bruno Fernandez avuliwe unahodha.

“Baada ya kumtazama tena ningemvua unahodha kwa asilimia 100. Najua ni uamuzi mgumu, lakini Fernandes sio nahodha.” Keane ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka alisema kupitia Televisheni ya Sky Sport.

“Ni mchezaji mwenye kipaji hakuna mjadala kuhusu hilo. Lakini nilichoona leo tumejadili mara nyingi kabla, ilikuwa msimu uliopita dhidi ya Liverpool, manung’uniko, kulalamika na kurusha mikono hewani kila mara haipendezi.” Alisema Keane.

Kauli ya Keane imekuja mara baada ya jana United kupoteza mchezo wa EPL dhidi ya Man City mabao 3-0 uwanja wa Old Trafford.

Habari Zifananazo

Back to top button