Royal Tour yaendelea kuleta wawekezaji

KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abasi amesema muitikio wa wawekezaji katika sekta ya utalii ni matokeo chanya ya filamu maalumu ya Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza utalii wa Tanzania.

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 18, 2023 katika Chuo cha Utalii, Posta Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa awali wa kibiashara ya uvunaji wa hewa ya ukaa nchini kati ya mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori (TAWA) na kampuni ya kigeni Green Cop Development (PTE).

Advertisement

Kwa upande wake Kamishna wa TAWA, Mabula Nyanda amesema katika kipindi hiki cha upembuzi yakinifu kuelekea utekelezaji mkataba huo, Tanzania italipwa Dola milioni 3.6 ambayo ni takribani Tsh bilioni 8.

Mabula ameongeza kuwa rasilimali zilizopo nchini ikiwemo misitu, ikolojia, maji na udongo ni muhimu kiuchumi na inafungua milango ya sekta binafsi kuwekeza

Hata hivyo uwekezaji huo mbali na faida za kifedha lakini pia kupunguzwa kwa hewa ya ukaa kunatarajiwa kutatua matatizo yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi kama mmomonyoko wa udongo, ukame na nyinginezo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *