RPC Geita aonya unyanyasaji dhidi ya wanaume

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP, Safia Jongo amewaonya wanawake wanaonyanyasa waume zao kuacha tabia hiyo kwani inapelekea watoto kukosa malezi sahihi ya wazazi.

Kamanda Jongo ametoa kalipio hilo leo wakati akizungumuza na wananchi wa kiijiji cha Lulembela kata ya Lulembela wilayani Mbogwe mkoani hapa na kusisitiza malezi dhaifu ndio kiini cha watoto kukengeuka.

Amesema utafiti aliofanya amebaini baadhi ya wanawake wananyanyasa na hata kupiga waume zao kwa kuwa wana uwezo wa kiuchumi na kusahau kuwa malezi ya watoto yanahitaji busara na hekima ya wazazi wote wawili.

Advertisement

Amewataka wanawake kuacha tabia hiyo na kuwekeza zaidi katika kujenga familia yenye malezi bora ili kuepuka kuwa na kizazi kilichokengeuka huku akiwataka wanaume kuwa wawazi wanapokutana na adha ya vipigo majumbani.

“Mwanamke anapiga mme mpaka anamfukuza kwenye nyumba, wanaume mnapigwa hamtaki tu kusema mnaona aibu, mnapigwa na mnafukuzwa ndani ya nyumba na mimi nimeshuhudia.

“Sasa unavyopiga mwanaume unamfukuza ndani ya nyumba, sawa una uwezo wa kulea huyo mtoto wewe mwenyewe, lakini huyo mtoto unayemlea atakosa malezi ya baba, na mwisho wa siku unapata mtoto kibaka.”

Aidha amekemea tabia ya wanaume kutelekeza familia zao na kuwataka kuwajibika kutoa huduma stahilki ndani ya familia kuepuka watoto kuingia kwenye tamaa na vishawishi vya matendo ambayo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *