RPC Kigoma awafunda madereva

POLISI mkoani Kigoma ikiongozwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Filemon Makungu wamevamia Kituo Kikuu cha mabasi mkoani Kigoma kufanya ukaguzi na kuzungumza na madereva wa mabasi yanayofanya safari nje ya mkoa.

Akizungumza na madereva wa mabasi ya abiria na abiria waliokuwa wakisafiri na mabasi hayo, Kamanda Makungu alisema kuwa ajali nyingi za barabarani zinaepukika na kubainisha kuwa uzembe wa madereva ndiyo chanzo kikuu cha ajali hizo.

Kamanda Makungu alisema kuwa ulevi wa madereva, mwendo kasi usiozingatia taratibu za usalama, ubovu wa gari unaojulikana na kuendesha gari mwendo mrefu huku dereva akiwa peke yake ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya ajali.

Habari Zifananazo

Back to top button