RPC Mbeya awataka wanafunzi kufichua uhalifu
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga amewataka wanafunzi mkoani humo kutokaa kimya dhidi ya vitendo vya uhalifu.
RPC Kuzaga ametoa maelekezo hayo alipotembelea shule ya msingi Azimio iliyopo mkoani humo ambapo ametoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la nne kuhusiana na masuala ulinzi na usalama.
Kamanda huyo amewasisitizia wanafunzi hao kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu kwa walimu, wazazi na jeshi la polisi ili hatua za haraka zichukuliwe.
Akizungumza na wanafunzi hao leo Oktoba 24, 2023 kamanda Kuzaga amewataka kujiepusha na makundi yasiyofaa na badala yake wajikite katika masomo kwa kuhakikisha wana somo kwa bidii na kufaulu.