RPC Shinyanga ataka ulinzi shirikishi

KAMANDA Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi, amesema watahakikisha kunakuwepo ulinzi shirikisho wa kutosha, kwani kuna matukio ya mimba za utotoni, kubakwa na vipigo kwa wanawake, pamoja na mauaji ya wazee yanayofanywa  kimyakimya.

Kamanda Magomi ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  Kata ya Mondo, Wilaya ya Kahama na kushirikisha  viongozi wa kimila na ulinzi wa jadi wa sungusungu katika vijiji vitano vya Bumbiti, Mondo, Mwanzwagi, Penzi na Sangilwa,  huku akiwataka wasimamie ulinzi na kutoa taarifa kwenye jeshi la polisi.

“Nimekuja muda mchache  mkoa wa Shinyanga, lakini mauaji yametokea kwa wilaya ya Kishapu na Ushetu ya wazee kwa imani za kishirikina, mimba za utotoni na vipigo,  nawaomba wanawake fungukeni na viongozi msikae kimya,” alisema Kamanda Magomi.

Amesema kuwa hivi sasa jeshi la polisi limekuja kivingine, ndiyo maana viongozi wa jeshi hilo, wanapita kwenye kila eneo, kuangalia hali ya ulinzi na usalama na wananchi msichukue sheria mkononi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button