Rubani wa burudani mwenye ndoto kimataifa
MWANAIDI Msuya maarufu kama ‘Dj Sweetlady’ anayejihusisha na shughuli ya uchezeshaji wa muziki amesema anajipanga kuwa Dj wa kimataifa huku akiwataka wadau kuendelea kumuunga mkono.
DJ huyo alijipatia umaarufu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchezesha muziki kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani ya mwaka 2015 hapa nchini.
Katika kampeni hiyo, Dj huyo alikuwa akizunguka na timu ya kampeni ya Chama cha Mapinduzi(CCM) iliyokuwa ikimnadi Mgombea wa urais John Magufuli ambaye mgombea mwenza alikuwa Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan
Kwenye kampeni hiyo DJ huyo alikuwa akichezesha muziki kwa wasanii waliokuwa kwenye kampeni hiyo, pamoja na kucheza nyimbo kadhaa za kampeni kwenye mikutano mbalimbali ya hadhara.
Dj Sweet lady alionesha uwezo mkubwa wa kuchezesha muziki hatua iliyopelekea kuajiliwa kwenye Kampuni ya Africa Media Group inayomiliki kituo cha Habari cha Luninga cha Chanel Ten pamoja.