Ruganzu waishukuru serikali mradi wa maji

WANANCHI wa Kijiji cha Ruganzu Wilaya ya Biharamulo, wameishukuru kwa jitihada za kumtua ndoo mama kichwani, baada ya kuanzisha miradi mbalimbali ya maji vijijini.

Akizungumza kijijini hapo, mmoja wa wanakijiji, Mwajuma Khamis, amesema baada mradi wa maji Ruganzu, Kata Nyanza, kuanza kutoa maji, umewaepushia adha kubwa waliyokuwa nayo katika miaka yote waliyoishi katika kijiji hicho.

Walisema serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, inaonesha na kwa jinsi gani serikali inavyowajali wananchi na kwamba hatua ya kuimarisha Ruwasa na kuipa bajeti ya kutosha kuhudumia wananchi, imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa kero ya maji vijijini.

Amesema kwa sasa wanatumia muda mchache kufuata maji, wakati miaka ya nyuma suala la maji lilikuwa likichukua muda wao mwingi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022, Sahili Geraruma, amewasihi wananchi wa Wilaya ya Biharamulo kuunga mkono juhudi za Rais Samia kwa kuunganisha huduma ya maji katika nyumba zao, hiyo itakuwa ndiyo maana halisi ya kumtua mama ndoo kichwani.

Akizungumza na wananchi, mara baada ya kuzindua mradi wa maji Ruganzu, uliojengwa na Shirika la CBHCC na nguvu za wananchi, ameshauri wananchi hao baada ya mradi kukamilika ni vyema sasa waunganishe huduma ya maji katika makazi yao.

“Ili kuunga juhudi za Samia kumtua mama ndoo kichwani, yatupasa kuunganisha huduma ya maji katika nyumba zetu, lakini kumuacha mama aendelee kufuata maji mita 200 au 300, tunakuwa bado hatujatimiza lengo la kumtua mama ndoo kichwani.

“Hivyo nawasihi wananchi tuhakikishe kila mmoja wetu anaunganisha huduma ya maji katika makazi yake, kwani kwa sasa gharama zimepungua sana ,” alisema  Geraruma.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x