Ruksa kujenga makumbusho binafsi

IRINGA: WIZARA ya Maliasili na Utalii imewataka wadau wa utalii na wananchi kuanzisha Makumbusho binafsi ili kurithisha tamaduni zao za masimulizi katika jamii zao.

 

Akifungua maonesho mapya kwenye Makumbusho ya Mkoa wa Iringa, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale, Mhifadhi Mkuu Idara ya Mambo ya Kale Prisca Kirway ametolea mfano wa juhudi zilizofanywa na Makumbusho ya Mkoa-Iringa.

“Sera ya Malikale ya mwaka 2008 inatoa ruksa kwa jamii kubuni na kuanzisha Makumbusho mbalimbali ili kurithisha mambo ya jamii zao,” amesema Kirway.

 

Onesho jipya lililozinduliwa katika Makumbusho hiyo kupitia programu ya ‘Fahari Yetu’ linaelezea masimulizi ya kusimumua kutoka katika jamii za mkoa wa Iringa na Njombe.

 

Amesema, Idara ya Mambo ya Kale chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika uhifadhi wa utajiri mkubwa wa urithi wa kihistoria na malikale nchini.

Idara hiyo pia inaendelea kuhamasisha wadau wa Malikale kuongeza mazao mapya ya Utalii nchini ili kuenda sambamba na matokeo chanya ya kazi nzuri ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya The Royal Tour.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button