DUNIA ikiwa inaungana katika kuomboleza msiba wa Malkia Elizabeth II, baadhi ya wakuu wa nchi wameshawasili Lancaster House, jijini London, nchini Uingereza kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia huyo.
Kutoka Afrika ya Mashariki, ukiachia Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alifika jijini humo na kusaini kitabu cha maombolezo, Rais wa Kenya, William Ruto naye amewasili jijini humo kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia.
Malkia Elizabeth II alifariki Septemba 8, 2022 na Mazishi yake yatafanyika leo Septemba 19, 2022 jijini London.
Ibada ya mazishi yake itafanyika Westminster Abbey na kisha mwili wa marehemu kupelekwa kasri la Windsor kwa ibada ya kifamilia na watu wa karibu zaidi, hatimaye, maziko ya kibinafsi.
Jumla ya wageni 2000, viongozi 500 wa kigeni, wahudumu 4,000 watashiriki na mabilioni ya watu duniani kote wanatarajia kufuatilia maziko yake leo.