RAIS wa Kenya, William Ruto ameombeleza kifo cha Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa kwa kueleza namna alivyoguswa na kiongozi huyo mwenye sifa za kipekee.
Kupitia mtandao wake wa X (zamani twitter), Ruto ameandika “Waziri Mkuu Edward Lowassa alikuwa kiongozi anayeheshimika na mpenda maendeleo aliyefanya kazi kwa manufaa makubwa ya wananchi wa Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki”
Amesema, Serikali ya Kenya inaheshimu maisha mashuhuri aliyoishi, kazi yake na urithi tajiri aliouacha.
“Mungu aipe nguvu familia, Rais @SuluhuSamia na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika wakati huu wa majonzi.” Ameandika kiongozi huyo na kumalizia Buriani Ndugu Lowassa.