Ruto aombwa kutanguliza mageuzi ya kisiasa ya Sudan Kusini

Ruto aombwa kutanguliza mageuzi ya kisiasa ya Sudan Kusini

MWANAHARAKATI mashuhuri nchini hapa, Edmund Yakani amemtaka Rais wa Kenya, William Ruto, kutanguliza mageuzi ya kisiasa katika nchi hiyo akisema Kenya na Sudan Kusini zinafanana.

Yakani ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uwezeshaji Jamii kwa Maendeleo (CEPO), alitoa rai hiyo siku moja baada ya Rais Salva Kiir Mayardit kuwa mmoja wa wakuu wa nchi wa kwanza kutoka Afrika kukutana binafsi na rais mpya wa Kenya, Ruto.

Aliitaka serikali mpya ya Kenya kuipa kipaumbele Sudan Kusini katika shughuli zake za kikanda na kuahidi kushirikisha uongozi mpya wa Kenya kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya amani ya nchi hiyo yaliyohuishwa na kutiwa saini mwaka 2018.

Advertisement

“CEPO inahimiza uongozi wa kisiasa wa Kenya kutanguliza mchakato wa mpito wa kisiasa wa Sudan Kusini. CEPO iko tayari kujihusisha na shughuli za ushawishi na uongozi mpya wa Kenya kwa ushirikishwaji mzuri wa utekelezaji wa R-ARCSS,” alisema.

Yakani alinukuliwa na Sudans Post akisema, muhula wa rais wa Kenya unaanza kabla ya kipindi cha mpito cha miezi 24 nchini hapa na kwamba, mpito wa kisiasa wa Sudan Kusini una uhusiano wa moja kwa moja na uchumi wa Kenya.

“Muhula wa William Ruto kama Rais wa Kenya unatarajiwa kuchangia ipasavyo kwa utekelezaji wa kweli wa R-ARCSS. Uthabiti wa kisiasa wa Sudan Kusini una athari za moja kwa moja katika ukuaji wa uchumi wa Kenya,” alisema Yakani.

Akaongeza: “Mafanikio ya biashara ya kikanda yanaamuliwa na mafanikio ya amani na usalama wa kanda. Kwa hivyo, ni muhimu kwa Rais William Ruto kupata utekelezaji wa kweli wa R-ARCSS kwa kuwa Sudan Kusini inatoa fursa kubwa ya biashara ya Kenya kupata faida.”

 

 

 

 

 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *