Ruto azindua mfuko wa Ma-Hustler

Rais wa Kenya, Dk William Ruto amezindua rasmi Mfuko wa ma-Hustler, mpango uliokuwa moja ya nguzo kuu za kampeni yake.

Ilikuwa kamari yake kubwa zaidi, na utekelezaji wake baada ya kuchaguliwa kuwa Rais – inathibitisha kuwa kamari kubwa zaidi kuwahi kuongelewa nchini Kenya.

Rais Ruto alianzisha kampeni yake kama “hustler” katika jaribio la kuondokana na uhamasishaji wa kawaida wa kikabila na kikanda.

Advertisement

Aliahidi kutoa Sh bilioni 50 za Kenya kwa ajili ya kuanzisha Mfuko huo maalumu kwa ajili ya vijana na yeye akijibatiza Mpambanaji Mkuu “Chief Hustler”.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *