Ruto, Museveni wamuunga mkono Odinga

KISOZI, Uganda: RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Kenya, William Ruto wameafikiana kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya na Kiongozi wa Chama cha upinzani cha Azimio la Umoja, Raila Odinga juu ya azma yake ya kuwania Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU)

Maafikiano hayo yamefanyika jana katika mualiko maalum wa Rais Museveni, shambani kwake Kisozi nchini Uganda.

Mbali na hayo, viongozi hao pia wamezungumzia hatua za makusudi zinazopaswa kufanyika ili kuimarisha ushirikiano wa Umoja wa Afrika Mashariki (EAC).

Habari Zifananazo

Back to top button