Ruto, Tshisekedi kushuhudia sherehe za Muungano

DAR ES SALAAM: Marais, William Ruto (Kenya), Felix Tshisekedi (DRC), Evariste Ndayishimiye (Burundi) ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria sherehe za miaka 60 ya Muungano kesho.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amewataja viongozi wengine watakaohudhuria ni Rais wa Comoros Azali Assoumani , Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na Rais wa Namibia Nangolo Mbumba.

Viongozi wengine ni Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima, Makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo na Waziri Mkuu wa Msumbiji Adriano Afonso Maleiane miongoni mwa viongozi wengine.

Habari Zifananazo

Back to top button