RAIS mteule William Ruto amesema utulivu uliopo nchini Kenya baada ya Uchaguzi wa Agosti 9 ni kwa neema za Mungu.
Akizungumza mjini Njoro Jumapili, Ruto amesema Wakenya haswa katika eneo la Rift valley walikuwa na sababu ya kumshukuru Mungu kwa amani na utulivu baada ya uchaguzi.
“Hii ni ibada yetu ya Jumapili ya tatu baada ya Kenya kwenda kupiga kura na ni ya kwanza kuwa nayo Rift Valley. Sisi sote kama wakazi wa Rift Valley tuna sababu ya kumshukuru Mungu,”