Ruvuma kupimwa afya bure

BALOZI wa China nchini Tanzania Chen Mingjian kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wamezindua utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma
Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 8 katika uwanja wa Majimaji Mjini Songea.
Huduma hizo za afya ambazo zitahusisha upimaji wa afya, matibabu na utoaji wa dawa zitatolewa na timu ya madaktari kumi kutoka nchini China kwa kushirikiana na madaktari wa Tanzania kutoka hospitali mbalimbali mkoani Ruvuma.
Huduma hizo zitatolewa Kwa muda wa siku tatu kuanzia leo November 8.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Kanali Thomas amewahimiza wananchi kujitokeza ili waweze kupima afya zao, kupata ushauri wa kiafya na kupatiwa matibabu bure kwa wale ambao watagundulika kuwa na tatizo la kiafya.

Madaktari wa China watashirikiana na madaktari wa Tanzania kutoa huduma ya matibabu  wenye magonjwa ya sukari, presha na magonjwa mengine.

Habari Zifananazo

Back to top button