Ruwasa yapeleka raha Kagera

KAGERA: Wakala wa maji na usafi na usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera imeanza kutekeleza agizo la Waziri wa Maji Juma Aweso alilolitoa mkoani Kagera Julai mwaka huu katika ziara yake na kuhakikisha vijiji vinavyozungukwa na ziwa Victoria vinanufaika na maji ya ziwa hilo.

Kamati ya ulinzi na usalama wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Wilison Sakulo alifanya ziara katika mradi wa maji wa Kashenye unaotekelezwa kutoka ziwa Victoria kwa Wilaya ya Missenyi na kupongeza jitihada za Ruwasa za kuhakikisha wananchi wa Kata za Kashenye ,Kanyigo na Bwanjai zinaanza kunufaika na mradi huo mkubwa wa maji.

Alisema kuwa kama wataalamu wataridhia basi mradi huo unufaishe na Kata nyingine ya Bugandika ambayo nayo iko jirani na kata hizo ili kuwafanya wakazi wa kata hiyo kuwa sehemu ya Furaha huku akiwataka wananchi kuhakikisha wanatunza miradi ya maji ya miundombinu ikiwa ni pamoja na kujiepusha na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.

Miradi mingine iliyotembelewa ni mradi wa maji Ishunju,na mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji wa kibeo yote kwa pamoja ikiwa ni hatua ya serikali kuongeza upatikanaji wa maji hadi kufikia asilimia 85 ifikapo mwaka 2025 kwa wananchi wanaoishi vijijini.

Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Missenyi Andrew Kilembe alisema kuwa mradi wa maji yanayotoka ziwa Victoria utanufaisha wananchi wapatao 23,319 ambapo mradi utakamilika kwa awamu ya kwanza April mwaka huu ambapo awamu ya kwanza ikikamilika itahudumia wakazi wa kata Kashenye na awamu ya pili itahudumia kata za Kanyingo na Bwanjai.

Alisema kuwa mpaka Sasa mradi huo umefikia asilimia 70 na awamu ya kwanza na unatekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 1.8 na mpaka sasa mkandarasi amelipwa zaidi ya Sh milioni 900.

Alitaja kazi za mradi zinazoendelea kukamilisha kuwa ni ujenzi wa tanki ujazo wa Lita 200,000 ambao umefikia asilimia 85, ujenzi wa Sump tank lenye ujazo wa lita 50,000 asilimia 70 pamoja na ujenzi wa ofisi ya jumuiya ya watumia maji ngazi ya jamii (CBWSO) umefikia asilimia 20.

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
yojisob442
20 days ago

I’am making over $15k a month working online. I kept seeing how some people are able to earn a lot of money online, so I decided to look into it. I had luck to stumble upon something that totally changed my life. After 2 months of searching, last month I received a paycheck for $15376 for just working on the laptop for a few hours weekly. I was amazed how easy it was after I tried it copy below web…www.work.profitguru7.com

Antoinetteopez
Antoinetteopez
20 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 20 days ago by Antoinetteopez
Angila
Angila
19 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions……
.
.
.
On This Website……………..> > W­w­w.S­m­a­r­t­c­a­r­e­e­r­1.c­o­m

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x