Saba wauawa majibizano ya risasa DR Congo
TAKRIBANI watu saba wameuawa katika majibizano ya risasi na waasi wa M23 huko Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DR Congo.
–
Mazingira yanayozunguka ufyatuaji risasi huo, ambao ulifanyika katika eneo la Nyiragongo, katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao Kaskazini mwa mji Mkuu wa Mkoa wa Goma, hauko wazi.
–
Kulingana na msimamizi wa polisi wa eneo hilo, Kanali Patrick Iduma, wanamgambo “wa kiasili” walifyatua risasi “kuwatia hofu watu waliokimbia makazi yao waliokuwa wakimiliki viwanja vyao”.
–
Kulingana na rais wa jumuiya ya kiraia ya eneo hilo wahalifu “walikuwa wamevalia sare mpya za askari. Aliongeza kuwa waliofariki ni pamoja na raia waliokuwa kwenye baa.