SACP Kaganda aapishwa

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillius Wambura, leo Oktoba 28, 2022, amemuapisha SACP Suzan Kaganda, kuwa Kamishna wa Polisi na Kamishna wa Kamisheni ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu.

Kaganda aliteuliwa na Rais Samia Suluhu  Oktoba 24, 2022 akichukua nafasi ya  Kamishna wa Polisi (CP), Benedict Wakulyamba ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Kaganda, alijipatia sifa alipotahadharisha askari kuacha kutumia bunduki kudai rushwa kwa madereva na wageni.

Advertisement

Ana uzoefu wa uongozi katika Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Juni, 2011 hadi Februari 2012 alifanya kazi akiwa Mkuu wa Kituo cha Polisi.

Kati ya mwaka 2013 hadi 2015 alikuwa Kamanda wa Polisi katika maeneo mbali mbali ikiwemo Tabora na Kinondoni na kuanzia Julai 2015 amekuwa Ofisa wa Jeshi la Polisi.

Anauzoefu katika masuala mbali mbali yakiwamo ya lojistiki, ugavi, uhusiano na mawasiliano kwa umma, upelelezi binafsi na pia ni mtaalamu wa masoko.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *