Safari ya miaka 36 TAMWA raha tu!

DAR ES SALAAM: CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeelezea mafanikio yake lukuki waliyopata katika miaka 36 ya kuanzishwa kwa chama hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dk Rose Reuben amesema katika miaka 36 Tamwa iliweza kushawishi Bunge la Jamhuri ya Muungao wa Tanzania mwaka 1998 likatunga sheria ya masuala ya kujamiiana SOPSA.

“Lengo ni kuzuia ukatili na kulinda heshima, hadhi, utu na haki za wanawake na watoto, inajulikana kama ‘The Sexual Offences Special Provisions Act of 1998 (SOPSA),”amesema Rose

Amesema,pia katika safari ya TAMWA ya miaka 36 iliweza kuanzisha gazeti la ‘Sauti ya Siti’lililoibua masuala ya uchunguzi na utafiti na Makala hizo ziliandikwa na waandishi wanawake na wanaume.

“Kadiri siku zilivyokwenda watu binafsi, taasisi, asasi, serikali na wadau wengine walianza kuunga mkono jitihada za TAMWA kupiga vita ukiukwaji wa haki za binadamu kwa mtazamo wa kijinsia,”amesema.

Pia, amesema kuondolewa kwa sheria ya wanawali mwaka 1985 ambapo msichana akipata mimba alifungwa jela na kama ni mwanafunzi hakuruhusiwa kurudi tena kusoma shule.

“Sheria hii iliondolewa kwa jitihada na ushawishi wa Rais Samia Suluhu Hasan, ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri wa Zanzibar anayeshughulikia dhamana ya masuala ya kijinsia, alibeba tatizo hilo hadi hatimae ile sheria ikafutwa,”amesema Dk Rose

Aidha, amesema TAMWA inaendelea kutumia vyombo vya habari kuhamasisha na kushawishi ili kuwatia moyo wanawake na vijana waliokuwa tyari kugombea nafasi za kuchaguliwa za kisiasa.

“Mafanikio ya TAMWA hayapo katika kutekeleza miradi tu lakini pia tunajivunia kuwapa elimu wanahabari hapa nchini pamoja na kuhamasisha kuwekwa kwa sera ya jinsia ndani ya vyombo vya habari,”amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button