Abiria wakwama Uwanja Ndege Abuja

Safari kadhaa za ndege zimesitishwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe katika mji mkuu wa Nijeria, Abuja baada ya ndege kutua kwa dharura na kuziba njia ya kurukia.

Ndege ya Max Air 737-400 ilipasuka tairi siku ya Jumapili ilipotua Abuja, kutoka Yola, Kaskazini-Mashariki mwa Jimbo la Adamawa.

Uongozi wa Max Air ulisema kuwa abiria wote 143, akiwemo mtoto mchanga na wafanyakazi sita ndani ya ndege hiyo waliondolewa salama bila kujeruhiwa.

Tukio hilo lilisababisha kuahirishwa kwa safari nyingi na ucheleweshaji kote nchini, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Abiria wengi wameripotiwa kukwama katika uwanja huo wa ndege.

Habari Zifananazo

Back to top button