Sagini akoshwa na maendeleo ya mradi Mtwara

MTWARA; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amesema kuwa, kukamilika kwa mradi wa jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara utaipa heshima na hadhi Ofisi ya Kamanda wa Polisi kwani kila Kitengo kitakuwa na ofisi yake tofauti na ilivyo kuwa sasa.

Sagini ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa Ujenzi wa Jengo la hilo katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya Sh bilioni 1.4  novemba 17 2023

“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni sikivu na nimearifiwa kuwa, fedha za awamu ya pili na tatu tayari zimetoka hivyo basi nimuombe mkandarasi kukamilisha ujenzi kama inavyoelekeza ili ofisi ianze kutumika.” Alisema

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Salim Morcase, amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ufuatiliaji wa karibu wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara.

“Sisi kama Jeshi la Polisi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kwako kwa ufuatiliaji wa karibu wa mradi wa ujenzi wa jengo letu”. Alisema ACP Morcase

Aidha, amebainisha kuwa, mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 92 na ulianza kutekelezwa Novemba 18, 2021 na unakadiriwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2023.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
15 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions….
.
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x