Sagini azindua mfumo wa kidigitali wa huduma za fedha Jeshi la polisi

DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi nchini leo Septemba 30, 2023 limezindua Mfumo wa kidijitali wa huduma za kifedha uitwao (URA MOBILE MONEY) utakaotumika na Viongozi pia Wanachama wa URA SACCOS katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Jijini Dar es Salaam, 2023.

Akizungumza katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Mfumo huo Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kutambua umuhimu wa kuwa na huduma za kifedha zinazotolewa na kupatikana kwa gharama nafuu kwa Watumishi wake na hivyo kuanzisha Ushirika wa kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) miaka 17 iliyopita.

“Nafahamu kama ilivyoelezwa kwamba, tangu kuanzishwa kwa Ushirika huu Tarehe 6 Septemba 2006, na kuutambua katika Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi (P.G.O 212) fursa mbalimbali zimetolewa kwa Watumishi kama vile uwekaji wa akiba na utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu ukilinganishwa na taasisi nyingine za kifedha,” amesema Sagini.

Pia amesema kuwa uwepo wa URA SACCOS umechangia ustawi wa Watumishi kiuchumi, kurahisisha utendaji, kuongeza ufanisi katika kazi na kuongeza heshima kubwa kwa Watumishi wa Jeshi la Polisi kwa kuboresha maisha na kuwaepusha kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa pindi wanapokabiliwa na mahitaji ya kifedha kwa ajili ya maendeleo yao.

“Kwa kufanya hivi mmeunga mkono kwa vitendo juhudi za Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais,Samia Suluhu Hassan ambaye kwa nyakati tofauti amesisitiza kuwekeza kwenye matumizi ya Tehama katika utekelezaji wa majukumu ya Umma,” amesema. Sagini.

Pia Naibu Waziri Sagini alimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Bodi ya URA SACCOS na watendaji wa URA SACCOS kwa ubunifu, ueledi na umahiri wa kukivusha Chama kutoka kwenye mfumo wa analojia kwenda kwenye kidigitali kwa lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
EmeraldEartha
EmeraldEartha
2 months ago

I’m currently generating over $35,100 a month thanks to one small internet job, therefore I really like your work! I am aware that with a beginning capital of $28,800, you are presently making a sizeable quantity of money online.( 33w)
Just open the link——->> http://Www.SmartCareer1.com

AnneThomas
AnneThomas
2 months ago

My last salary was $8,750 only worked 12 hours a week. My longtime neighbor estimated $15,000 and works about 20 hours for seven days. I can’t believe how blunt he was when I looked up his information.
.
.
Detail Here—————————————————————->>>  http://Www.BizWork1.Com

Lisa D. Nelson
Lisa D. Nelson
2 months ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 2 months ago by Lisa D. Nelson
MAPESA1234567
MAPESA1234567
2 months ago

HE/SHE DIED WITH CARDINAL RUGAMBWA HOSPITAL “CONFERENCE” DISEASE… THE HISTORY OF THIS DISEASE WAS KILLED MORE THAN 5 MILION PEOPLE AROUND THE WORLD MANY WAS CHINESE, EROPEAN, KOREAN AND INDIANS… ALL WHERE WHITE SKIN PEOPLE

Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x