Saka aondolewa England

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Bukayo Saka ameondolewa kwenye kikosi cha England kinachojiandaa kufuzu mashindano ya Euro dhidi ya Australia na Italia kutokana na majeraha.

Saka alikosa ushindi wa 1-0 wa timu yake dhidi ya Manchester City Jumapili kutokana na jeraha la misuli ya paja.

Shirikisho la soka England ‘FA’ limethibitisha nyota huyo kuondolewa baada ya kufanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari ya Uingereza.

England itamenyana na Australia tarehe 13 Oktoba, kabla ya kukutana na Italia katika mechi ya kufuzu kwa Euro siku nne baadaye.

Habari Zifananazo

Back to top button