Sakata la mahindi, Spika atoa agizo kwa serikali

SPIKA Bunge, Dkt. Tulia Ackson ameiagiza Serikali kuweka wazi kiwango cha mahindi ambacho Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaweza kununua ili kuweka urahisi kwa wananchi kuweza kuuza mahindi nje.

Dkt. Tulia ametoa agizo hilo baada ya kuibuka kwa hoja bungeni kuhusu utaratibu wa kununua mahindi ambapo baadhi ya wabunge wamesema kuwa NFRA haijaanza kununua mahindi, hali inayowaumiza wananchi.

Hoja hiyo ilifanya ratiba ya shughuli za bunge kuhairishwa kwa muda ili kujadiliwa kwa suala hilo la utaratibu wa kusafirisha mazao hayo kwenda nje ya nchi.

Advertisement

Wabunge walidai kuwa licha ya Serikali kutoa  maagizo kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuanza kununua mazao, baadhi ya maeneo zoezi hilo halijaanza.

Maagizo hayo yamekuja baada ya jana Juni 22, 2023 serikali kusisitiza kuwa haijazuia usafirishaji wa mazao nje ya nchi, lakini badala yake imezuia usafirishaji mazao nje ya nchi kinyume na utaratibu.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *