Salah arejea mazoezini

LIVERPOOL, England: Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah amerejea mazoezini leo huku timu yake ikijiandaa kuikabili Manchester City siku ya Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Majogoo wa Anfield watawakaribisha Man City katika mchezo unatazamiwa kuwa wa maamuzi ya mbio za ubingwa wa ligi hiyo pendwa ulimwenguni.

Salah amekosa mechi nne za mwisho za Liverpool kutokana na majeraha,            msimu huu amefunga mabao 19 na kuhusika kutengeneza mengine tisa.

Advertisement

Timu hizo mbili zinachuana vikali katika mbio za ubingwa Liverpool wakishika usukani wa Epl na alama 63 huku mabingwa watetezi wa ligi hiyo wakikamata nafasi ya pili na alama zao 62 kibindoni.