Salah haamini kukosa UEFA

NYOTA wa Liverpool ‘The Reds’ Mohamed Salah amesema “Nimefadhaishwa” ni baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Salah ‘ametweet’ nakusema kuwa “Hakuna udhuru kabisa kwa hili. Tulikuwa na kila kitu tulichohitaji ili kufikia Ligi ya Mabingwa msimu ujao na tukashindwa, sisi ni Liverpool na kufuzu kwenye mashindano hayo ni jambo dogo sana.” Ameandika Salah.

Ndoto za Liverpool kucheza Ligi ya Mabingwa zilizimwa jana na Manchester United baada ya kuifunga Chelsea mabao 4-1 na kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye ligi hiyo msimu ujao na kuzima matumaini ya Liverpool kushiriki kwenye michuano hiyo.

Advertisement

Hii inamaana Liverpool watashiriki Ligi ya Europa huku mara ya mwisho kufanya hivyo ikiwa ni msimu wa mwaka 2015-16.