Salah nje mwezi mmoja

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohammed Salah huenda akawa nje ya uwanja kwa siku 21-28 kutokana na jeraha alilolipata katika mchezo wa Afcon kati ya Misri na Ghana.

Taarifa iliyotolewa na wakala wa mchezaji huyo, Ramy Abbas imeeleza kuwa “Jeraha ni kubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa”.

“Nafasi yake nzuri zaidi ya kushiriki AFCON ya sasa ni kwa kufanyiwa ukarabati mkubwa nchini Uingereza na kujiunga na timu mara tu atakapokuwa fiti”. Ameeleza wakala huyo.

Salah atasafiri kwenda Uingereza kuungana na Liverpool na kuanza haraka kupatiwa matibabu.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button