Saliba uhakika mkataba mpya

MKAKATI wa Arsenal kuendelea kuwapa mikataba mipya baadhi ya nyota wao unaendelea, baada ya kuripotiwa beki William Saliba anakaribia kuongeza mkataba mpya.

Taarifa ya mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano imeeleza nyaraka za mkataba zimethibishwa kuwa Mfaransa huyo atasaini mkataba wa miaka mitano wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.

Romano amesema mkataba wa Saliba utaisha 2027 kwa mujibu wa nyaraka hizo. Arsenal tayari imewaongezea mikataba mipya, Bukayo Saka, Gabriel Martinell na Gabriel Magalhães.

Imeelezwa Martin Odergaad na Neiss Nelson wanajiandaa kuongeza mikataba mipya.

Habari Zifananazo

Back to top button