BEKI wa Arsenal, William Saliba ameongeza mkataba wa miaka minne wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo nchini Italia, Fabrizio Romano, Saliba alikubali dili hilo tangu mwezi Juni.
Mkataba huo wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja, utaisha Juni 2027.
Mfaransa huyo alisajiliwa na Arsenal mwaka mwaka 2019 akatolewa kwa mkopo Saint-Étienne, baadaye alijiunga na Nice kwa mkopo kisha Marseille na kurejea London.