Samaki waanza kupatikana kwa wingi Dar es Salaam

SAMAKI aina ya tasi, jodari, mizia na dagaa mchele wameanza kupatikana kwa wingi katika Soko la Samaki la Kimataifa Dar es Salaam.

Ofisa Uvuvi Mwandamizi Ramadhan Mtabika katika soko hilo, amesema hayo alipozungumza na HabariLeo.

Mtabika amesema upatikanaji wa samaki hao ni kutokana na mvua kupungua hivyo wavuvi wengi kwenda baharini kuvua.

Advertisement

” Kuanzia mwishoni mwa Januari mwaka huu hadi sasa mvua zimepungua na wavuvi wengi wanaenda kuvua.

“Ongezeko la samaki limeanza kuonekana, samaki aina ya tasi, jodari, mizia na dagaa mchele,” amesema.

Amesema kwa sasa ndoo ya kilo 20 ya dagaa mchele ni kati ya sh 60,000 hadi 70,000 tofauti na samaki walioojuwa adimu walikuwa ni sh 90,000 hadi 95,000.

Amesema samaki aina ya changu kilo iliuzwa zaidi ya sh 10,000 lakini hivi sasa kilo ni sh 9000 hadi 10,000.