Samatta atwaa ubingwa Ligi Kuu Ugiriki
ATHENS, Ugiriki: NAHODHA wa @taifastars_ Mbwana Samatta @samagoal77 ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Ugiriki Msimu wa 2023/24.
Hilo ni taji la kwanza kwa Samatta nchini humo tangu ajiunge na Paok FC mnamo Agosti 2022, baada ya kuondoka Aston Villa ya England.
Aliondoka Aston Villa kwa mkopo kwenda Fenerbahçe ya Uturuki, baadae KRC Genk kabla ya kuhamia Paok FC.
Soma pia: https://habarileo.co.tz/samatta-atimkia-ugiriki/
Haya ni mafanikio makubwa kwake na ni furaha kubwa kuona wachezaji wa Tanzania wakifanya vizuri kimataifa. Natumai hii ni hatua moja tu kati ya mafanikio mengi zaidi kwa Samatta na kwa soka ya Tanzania kwa ujumla.