Samia afanya mabadiliko makatibu wizarani

ZANZIBAR: RAIS SAMIA amemteua Mhandisi Cyprian Luhemeja kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Kabla ya uteuzi huo, Luhemeja alikuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia pia amemteua Edwin Mhede kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, akichukuwa nafasi ya Agnes Meena ambaye amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa DART.

Rais Samia amemteua, Dk Suleiman Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, kabla ya uteuzi huo Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya Simanjiro.

Serera anachukua nafasi ya Nicholaus Mkapa ambaye amehamishiwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Pia Rais Samia amehamisha Mary Maganga kutoka Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira kwenda kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Habari Zifananazo

Back to top button