RAIS Samia Suluhu Hassan ameteua viongozi kadhaa akiwemo Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus Alhamis ilieleza kuwa Balozi Maajar anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu, Damian Lubuva ambaye alimaliza muda wake.
Zuhura alieleza kuwa Rais Samia pia amemteua Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
“Profesa Anangisye anaendelea kwa kipindi cha pili.
Uteuzi huu unaanza tarehe 23 Agosti, 2022,” ilieleza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.