Samia ahamasisha Uwekezaji

PWANI: Rais Samia Suluhu Hassan, amesema milango ipo wazi kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza Tanzania katika harakati za kuendelea kukuza uchumi wa Taifa.

Rais Samia ameyasema hayo leo Septemba 20, 2023 Mkoa wa Pwani alipokuwa akizungumza na wananchi wa mkoa huo.

“Serikali imefanya maboresho mengi ya kisera na kikanuni, ili kuhakikisha mazingira ya uwekezaji na biashara yanakuwa bora zaidi,” amesema Rais Samia.

Amesema wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi hawapaswi kuwa na mashaka yoyote, kwani mali zao zitakuwa salama na na uwekezaji wao utakuwa na faida huku pia serikali ikifaidika kupitia kodi.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *